Saturday, November 29, 2014

NJIA SAHIHI YA KUMPATA MKE AU MUME KUTOKA KWA BWANA. by PASTOR SONGWA KAZI. CONTACTS; 0757-567 899, 0789-567 899, Email: ptrsongwak@gmail.comNJIA SAHIHI YA KUMPATA MKE AU MUME KUTOKA KWA BWANA.

Yaliyomo:
SHUKURANI
KUHUSU MWANDISHI - WASIFU
UTANGULIZI

1. CHANZO CHA NDOA NA KUSUDI LA NDOA

2. NJIA YA KUMPATA MKE AU MUME KUTOKA KWA BWANA

3. SABABU ZAINAZOFANYA KIJANA ACHELEWE KUOA AU KUOLEWA

4. MAMBO YA KUYAELEWA KATIKA MAHUSIANO

5. UTAJUAJE KUWA HUYU NI CHAGUO LAKO

6. MAMBO YANAYO VUNJA MAHUSIANO

7. MAMBO YANAYO JENGA MAHUSIANO

8. MAMBO YAKUZINGATIA ILI KUIMALIZA SAFARI YAMAHUSIANO SALAMA NA KWA USHINDI MKUU

9. MAOMBI


MAANDIKO YA MSINGI YA SOMO.

Mwanzo 1:26-28, Mwanzo 2:7,15,18-25 , Mithali 19:14 na Mithali 18:22

I. SHUKURANI.

Kipekee ninamshukuru Bwana Yesu kwa kunipa neema na kibali cha kutumika pamoja naye katika huduma hii ya Injili.Kwani pasipo msaada wake kazi hii njema isingeweza kutoka.

Pili nawashukuru wazazi wanu kwakunilea vizuri; hasa mama yangu mzazi kipenzi Rhoda Menga Kubagwa,aliyeko nyumbani Bunda-Mara. Mungu akubariki kwa malezi na maombi yako.

Tatu wachungaji wangu wapendwa na rafiki zangu walio nilea kiroho, kunifundisha , kunishauri, kunitia moyo na kuniombea; hata leo nakuletea kitabu hiki cha Njia sahihi ya kumpata umpendae, hasa wachungaji wote na baraza la wazee TAG-Ilala chini ya Mchungaji Dk. Titus Mkama,Mchungaji Abraham Masasi –TAG Bunju, Mathayo Muna-KLPT Tegeta, Mchungaji Ibrahim Songoro-TAG Mb/Rangi tatu, Akofu Jonas Laizer-TAG Ngarash Monduli ARS,Mch. Joseph M. Lukumay TAG –Liboisoiti Manyara,Mch. Isaya Kibhuyo -TAG Mbuyuni Arusha,Mch. Christopher-TAG Lashaine Monduli, Mch. Richard Tajiri-Mana For All Nations Church-Karatu,Mch Askofu Nickson Kalinga-BETHEL CHURCH na Askofu Amos Mdoe –TAG Kimanzichana, Mch. Mpupua-TAG Mkuranga, Mch. L.Mrisho-TAG Vikindu na Mch. D.Marecan-TAG Kisemvule

Nne pia na mshukuru Mungu sana kwa kunipa baba mzuri wa kiroho Mchungaji Victor A. Tawete-TAG Kongowe Forest aliye itambua huduma yangu na kunipa fursa yakutumia karama na vipawa kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo- Kanisa.

Tano namshukuru mke wangu mpenzi Miriam S. Kazi na watoto wangu wazuri Meshach na Prince kwa maombi na uvumilivu wao kwangu hasa pale walipo nikosa kwa sababu ya utumishi na kazi ya huduma ya Injili.

Sita,nawashukuru wachungaji na rafiki zangu wote kwa maombi, michango na ushauri wenu pale nilipohitaji, na kwa watenda kazi wenzangu na marafiki wa huduma yetu ya Life Changing Ministry International-LCM; Ev. Abraham Magoma,Ev. Julius Mugisha, Mch. Emanuel Francis-FPCT Ifakara, Ev. Oliver Shaibu, Mch. Christopher Mapunda TAG-Mbulu Kahama, Mary Mwati, Flora Kitula, Dismas Damas Nyungula, Festus.SK. Ruhoya, Hallington Kamanga, Mch. Emile Yotham, Mch. Samwel Pyuza MRC- Kongowe, Mch. Rwedina Chelelo, Mch. Yohana Batano –African Leadership National Director , Mch. Mathias John-EAGT Igombe Mwanza, Mch. Marko Kayumbo -MRC, GTP Team –TAG Ilala na Viongozi na watakatifu wote Wa TAG Kongowe Forest, na wote nisiyo wataja kwa majina Mungu awabariki kwa maombi yenu kwangu.

II. KUHUSU MWANDISHI.

Mtumishi Pastor Kazi ,alizaliwa huko Bunda –Mara mnano mwaka 1980 akiwa Mtoto wa kumi na wa mwisho-kitinda mimba katika familia. Na alizaliwa mara ya pili, yaani kuokoka mwaka 1999.

=ELIMU:

Elimu ya msingi aliipata katika shule ya msingi Mcharo iliyoko wilaya ya Bunda.

Elimu ya Sekondari –O’Level aliipata katika Sekondari ya Metropolis High. Technical & Commercial Schoool-Mbagala Dsm.

Elimu ya juu- A-Level aliipata kutoka Tegeta High Schoool-Dsm. Ana Cheti-Certicate cha Mitihani ya Bodi ya Biashara ya Taifa [ National Business Examinations-NABE-III.]

Elimu ya Biblia; Ana Cheti-[Certificate] chaTheolojia- Elimu kuhusu Mungu- Theology In Bible kutoka African Leadership Inernational-AL alichopata baada ya miaka 2 ½.[2011-2013]

Kwa sasa anachukua Shahada [digrii] katika Uongozi, Utawala na Huduma-[ Bachelor In Administration,management and Ministry-BA In Min] kutoka katika Chuo Cha Kimataifa cha T-NET INTERNATIONAL.

=HUDUMA.

-Kwa miaka takribani kumi na mbili [12] sasa amekuwa akifanya huduma za Umisheni-Umishenari, Uinjilisti na Ualimu katika maeneo mbalimbali ya Vijijini na Mijini ndani ya nchi na nje nchi pia kwa kujitoa-kidhabihu kwa gharama zake mwenyewe na wapenzi wa Injili hutoa vitu vyao ili kuwafikia watu wenye kiu na njaa ya haki-Injili bila kutazamia malipo, kwani tumepewa bure tutoe bure-Math.10:8, akihubiri na kufundisha Kweli ya Neno hai la Mungu-Sound Doctrine na amefanyika baraka kuu kila eneo alilofika kihuduma kwakulijenga kanisa na kuwaongoza watu wengi kumjua na kumwamini BWANA YESU na wengine wengi kufunguliwa kutoka kwenye vifungo na magereza ya utumwa wa nguvu za giza.

-Pia kwa takribani miaka tisa-9 sasa amekuwa akiandaa na kuendesha Mikutano ya Injili, Semina na Makongamano ya Uamusho na Matengenezo; ili Kuijenga na Kuinua Misingi ya Vizazi vingi. Isaya 58:12-14, Zab. 11:3 akishirikiana na huduma na makanisa rafiki ya mahali pamoja.

-Ni Kiongozi na Mkurugenzi Mkuu [ Director General] na mwasisi wa Huduma ya Life Changing Ministry International-LCM ; yenye malengo ya kuleta matengenezo na Uamusho-yaani kuinua Misingi ya Vizazi vingi na kuibua vipawa ,karama na huduma ili kumzalia Bwana matunda kwa kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi wa Yesu na hivyo kuukamilisha Utume Mkuu ambao ndio Amri na Agizo kuu la Kanisa-Math.28:18-20.

-Mwandishi kwa sasa ni Mchungaji Msaidizi Kanisa la TAG Kongowe Forest chini ya Mchungaji Victor Tawete, Ni Katibu wa Kamati ya Kupanda Makanisa wilaya ya Mkuranga-District Church Planting Commettee Secretary-CPC; Ni Makamu Mkurugenzi wa idara ya Uinjilisti-Wilaya [Disrtict Deputy Director For Evangelism Derpartment]; Ni mtunza hazina wa Idara ya Vijana-wilaya [Youth District DerpartmentTreasurer ]; Ni Mkurugenzi wa Idara ya Uanafunzi na Maandiko-Wilaya Mkuranga –District Disciple Literature Derpartment Director].

Pia kwa sasa ni Mwalimu wa English Medium School na Mwalimu katika Kituo Cha Wachungaji na Viongozi wa Kanisa-BTCP/L Chini ya Chuo cha African Leadership International

-Kitabu kingine alicho kiandika ni ‘ IJUE IBABA YA KWELI’ Toleo la kwanza.

Alifunga NDOA mwaka 2008 Agosti,26 na Miriam na Mungu amewabarikia watoto wawili wa kiume, Meshach na Prince. Bwana Yesu awabariki wote.

III. UTANGULIZI

Je, wewe ni miongoni mwa vijana walio na maono au ndoto ya kuoa ama kuolewa-yaani ndoto za kumpata mwenzi wa maisha umpendae?

-Na kama jibu lako ni ndio; basi kitabu hiki kitakufaa sana kukupa nuru na kukuongezea hatua zaidi ili uanze na kumaliza salama na vizuri safari au mbio za mahusiano ulizonazo au unazotazamia kuwa nazo siku za usoni.

-Pia hata kama umeoa au kuolewa ama umekwisha mpata umpendae na mnatazamia kufunga pingu za maisha –ndoa hivi karibuni bado kitabu hiki kitakuwa cha msaada sana kwako pia ili kukisaidia kizazi hiki kinachokabiliwa na changamoto nyingi za kila namna ili kisipotee na kisifanye makosa kwa kukosa maarifa-Hosea 4:6; kama wengine waliofanya makosa na wakaumia; hata sasa wanalia,wanajuta kwani walijiingiza kwenye wimbi hili la mahusiano bila kuwa na maarifa na ufahamu wakutosha.

Biblia inasema katika Hosea 4:6 kuwa, ‘ Watu wangu wanaangamizwa kwakukosa maarifa….’Hivyo sitaki na Mungu hataki kabisa wewe au kizazi chetu na kile kijacho kiangamizwe eti kwakukosa maarifa, ndio maana sasa kinakuja kitabu hiki ili kutupa maarifa , nyenzo na nuru katika maeneo fulanifulani ya mahusiano.

-Hivyo kitabu hiki ni silaha iliyo mkononi na nyezo tosha yakumsaidia kijana kutokufanya makosa yanayoweza kuepukika yatokanayo na makosa ya kukosa maarifa yaani ufahamu. Elewa kuwa UFAHAMU NI NGUVU.

-Kitabu hiki kinamfaa kila mtu mwenye ndoto au maono ya kwamba ipo siku moja atakuwa mke au mume wa mtu; Kwa msingi huo kitabu hiki kinafaa kusomwa na vijana, wanafunzi, wanandoa , watumishi na viongozi wote ili tusifanye makosa wakati utakapo wadia-fika wa kuoa au kuolewa.

-Hakikisha mtumishi mwenzangu unayo nakala hii kwenye makitaba yako ili kukisaidia kizazi chetu.

KUMBUKA:

Kuoa au kuolewa yaani NDOA ni mpango wa asili wa Mungu kwa kwetu sisi watoto wake. Tazama Mwanzo 1:26-28 hasa mstari wa 27-28 inasema, ‘ Mungu akaumba mtu kwa mfano wake,kwa mfano wa Mungu alimuumba, mwanamume na mwanamke, aliwaumba. Mungu akawabarikia, zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

KUMBUKA:

Mungu hapendezwi kuwaona vijana wenye umri na sifa za kuoa ama kuolewa hawajitambui [hawajaoa na kuolewa] . Mwanzo2:18; Bwana Mungu akasema , si vema huyo mtu awe peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Nini tunajifunza hapa? Ni kuwa Mungu ndiye BWANA wa historia na mwasisi wa taasisi hii ya NDOA, hivyo ni mpango mkakati wa Mungu kabisa wa kuoa na kuolewa.

Mithali 18:22 inasema, “ Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA.” Kwa lugha nyepesi Mungu ndiye anae toa kibali cha watu kuoa na kuolewa hii ni kuponyesha jinsi alivyo makini [ serious] na swala ndoa. Tazama pia Mithali 19:14 ina sema kuwa, “ Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.

Sasa karibu tuangalie kwa pamoja hazina iliyopo kwenye somo hili na Mungu wangu akutane na haja ya moyo wako katika jina la Yesu, Amen.

SURA YA KWANZA: CHANZO NA KUSUDI LA NDOA.

=CHANZO NDOA kuwepo sio wazo wala mpango wa mtu au kikundi fulani bali ni mpango mkamilifu wa Mungu mwenyewe; Na Mungu ndiye aliye fungisha ndoa ya kwanza, Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia , Mungu akasema, zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, nakila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”

-Kulithibitisha hili Mungu mwenyewe kupitia mtunzi wa Mithali 19:14 anasema; “…….mke mwenye busara mtu hupewa na BWANA” wala sio mtu, wazazi,marafiki n.k

=KUSUDI LA NDOA

>Kusudi ni ile sababu iliyopelekea jambo au kitu fulani kuwepo. Tangu mwanzo Mungu aliweka wazi kusudi la NDOA katika kitabu cha Mwanzo 1:28, alipo wabarikia Adamu na Eva, akasema, “ Zaeni Mkaongezeke…..”Hivyo moja ya kusudi la Ndoa ni:-

[i] Kuendeleza uzao-kizazi [ uumbaji] wa kiroho na kimwili; kwa maana ya kwamba Mungu asingeendelea kufinyanga tope siku zote ila aliweka mfumo ndani ya mwadamu kuendeleza kizazi.

[ii] Ushirika na kusaidiana majukumu endelevu, kwani Adamu alionekana kuwa yuko mpweke ndipo Mungu akasema si vyema huyo mtu – Adamu awe peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Mwanzo 2:18 na Mithali 19:14, anapo sema, “ Mke mwenye busara ( wise, understanding and prudent wife) ni aina ya mke atakaye weza kuwa na uwezo wa kulielewa kusudi la Mungu ndani yako na kuwa sehemu ya kulifanikisha, kuliendeleza na kulikamilisha; kinyume chake utakapokosea kumpata mke au mume mwenye busara-hekima atakuwa mwiba [kikwazo] mbavuni mwako na atatumika kikamilifu kukukwamisha kwenye utumishi na hata katika ndoto au maono ya maisha uliyo nayo.

KUMBUKA:

*Yupo mke/mume wa kupewa na BWANA

* Yuko mke/mume wakupewa na wazazi,ndugu au marafiki

* Yuko mke/mume wakujipatia mwenyewe

>Mke au mume atakae kufaa kati ya hao watatu na kulikamilisha kusudi la Mungu maishani mwako ni yule atokaye kwa BWANA- Mithali 19:14.

SURA YA PILI : NJIA SAHIHI YA KUMPATA MKE AU MUME KUTOKA KWA BWANA.

NJIA- Ni mwongozo au dira [direction] inayo mwongoza mtu kufika au kumaliza mwendo au safari yake vizuri bila kupotea. Hivyo kumbuka ; Kila njia ina masharti yake yaani taratibu au kanuni kwa hiyo yakupasa kuyafuata vema ili usikwame kupata ajari na kupotea njiani.

KUMBUKA:

Kama hujui unakokwenda, njia yoyote itakufikisha huko usikokujua. Ni sawa na kulenga hewa utafanikiwa kupiga shabaha hiyo, na hakuna anaye lenga hewa akaikosa.

Mathayo 15:14 ina zungumza kwa habari ya kiongozi kipofu akimongoza kipofu mwenzake wote watatumbukia shimoni. Hivyo lengo la Njia hizi ni ili usije ukatumbukia kwa kuwa kipofu bali uone sawasawa-uwe na ufahamu wakutosha juu ya mahusiano.

>Njia pekee yua kanisa yaani mwongozo wetu ni NENO la MUNGU kwani ndio lenye nuru yakutuongoza ili kumpata mke au mume sahihi umpendaye kutoka kwa BWANA.

Zifuatazo ni baadhi tu ya Njia hizo:-

[i] Jipate kwanza wewe mwenyewe vizuri.

Hii ina maana kabla ya kumpata mwenzi wa maisha au umpendae anza kwanza kujipata wewe mwenyewe-yaani ni ule uwezo wakujitambua –kujielewa vizuri kuwa wewe ni mke au mume wa mtu hata kabla ya kumpata umpendae.

-Hivyo kitendo cha kujipata mwenyewe ni ile hali au uwezo wa KIJITAMBUA, kujiweza mwenyewe ili usije ukawa mzigo huko uendako. Mwanzo 2:15-25 hapa tunaona Adamu anapewa majukumu na Mungu ya kuilima na kuitunza bustani ya Edeni kama kipimo cha kuya kabili majukumu ya familia. Sio unakuta muoaji na mwolewa wote hawajitambui; ikitokea wanaanza maisha ya ndoa na wakapata watoto ;utakuta mtoto analia , mama analia na baba naye analia hakuna hata mmoja wakumsaidia mwingine; na ndio maana tumeshuhudia matukio yakinyama katika nchi yetu na hata mataifa mengine ya watoto wachanga kutelekezwa na wengine kutupwa majalalani na hata kutumbukizwa chooni-maana yake aliingia kwenye mahusiano akiwa hajitambui na hajui nini kitatokea mbele ya safari; hili ni tatizo la kuwa na msingi mbovu wa ndoa. Kwa hiyo kwako wewe unaye kisoma kitabu hiki isikutokee kabisa. Kwani ndoa ikipona kanisa limepona.

KUMBUKA:

Tatizo kubwa la wachumba au wanandoa watarajiwa na wanandoa na kimo-yaani kiwango chao cha ufahamu juu ya tasisi [kitengo] hiki ni kidogo sana.

ANGALIZO:

-Kijana; Waone mabinti wote kuwa wazuri lakini usiwabinafsishe wote, wako ni mmoja tu.

-Mabinti; Waone vijana wote kuwa wazuri lakini usiwabinafsishe wote, yupo mmoja tu aliye wako.

* Hili tutaliangalia zaidi huko mbele kwenye kipengele cha “ Utamtambuaje aliye chaguo lako.”

Elewa kuwa;

Wanaume wote ni waume lakini sio wote ni waume zako, hali kadhalika wanawake wote ni wake lakini sio wote wake zako.

*Tembea ukijua wazi wewe ni mke au mume wa mtu au wewe ni jibu la mtu.

[ii] Usitafute mke au mume:

Kitabu cha Mwanzo 2:7,15,18-25 kinatupa picha kamili juu ya mchakato mzima wa kumpata umpendae. Hapa tunaona wazi Mungu ndiye aliye husika kwa asilimia zote wakumtafutia Adamu mke –mwenzi wa kufanana nae. Katika sura na mistari hii tunaona Mungu anampa Adamu wajibu wa kuilima na kuitunza bustani ya Edeni. Na popote palipo na wajibu lazima pawe na haki hali kadhalika na kinyume chake vivyo hivyo. Na kwa msingi huo hatumwoni Adamu akihangaika kutafuta mke huku na kule kama wengine wafanyavyo hivi leo, anachumbia huyu mara yule vurugu tupu, lakini hapa Adamu alitulia na kujikita kwenye wajibu [kazi] ya kuilima na kuitunza bustani ya Edeni na Mungu mwenyewe akaona si vema Adamu aendelee kuwa peke yake; akampa Eva wa kufanana naye.

-Hivyo wajibu wako kama mwana wa Mungu ni kuwa mtu wa Ibada wa viwango vya juu pamoja na kutumika nyumbani mwa Bwana kwa kadri ya nguvu alizokujalia Mungu.

KUMBUKA:

Hakuna mtu anayependa kuoa au kuolea na mtu mvivu-mlegevu-mzembe asiyejituma-asiye wajibika vema.

-Hivyo wewe jikite kikamilifu katika kumwabudu Mungu na kumtumikia kwa nguvu zako zote na kwa nia safi kabisa katika kanisa lako na swala la mke au mume mwachie Mungu alishughulikie; cha muhimu kwako mtangazie Mungu nia yako –yaani mwambie haja ya moyo wako yakuwa una maono au ndoto za kuoa au kuolewa kwani ukinyamaza,leo vijana wanasema inakula kwako maana yake utapata hasara mwenyewe. Kwanini nimesema hivyo ni kwa sababu wapo vijana wengi nimekutana nao hujifanya kuwa ni wakiroho sana na hulipuuza swala hili la kuoa na kuolewa na utakapo jaribu kuongelea jambo hili huondoka hata wasisikie na hao hao mwisho wa siku unasikia kapola au kampa binti wa watu mimba au kazini na kijana Fulani. Usilipuuze swala nyeti kama hili la mahusiano, funguka sema na Mchungaji wako sasa uwe wazi, eleweka na tangaza nia yako.

Kumbuka kuwa Mungu hujishughulisha sana na mambo yetu, hasa pale tunapo jitoa kikamilifu kwake, 2Petro5:7

[iii] Maombi na Shukurani.

>Neno linaweka wazi katika Wafilipi 4:4-7 kwamba tusijisumbue kwa jambo au neno lolote ; maana yake likiwemo hata hilo swala lako la kumpata umpendae, Biblia inasema, “Bali katika kila jambo kwa kusali na kuomba na kushukuru haja zako, [yaani mahitaji yako] zijulikane na Mungu.”

>Ni katika wakati wa maombi tunapo mjulisha Mungu haja zetu. Vijana wengi leo hawafanyi maombi kabla ya kumpata mwenzi wa maisha bali wanaomba baada ya kuwa wamekwisha kuona, hili tayari ni tatizo ni sawa na mtu anaye jitekenya mwenyewe na kisha kuanza kucheka.

>Hupaswi kuanza mahusiano kabla ya kufanya maombi.Tuomba ili tupewe kuona sawasawa yaliyo mapenzi ya Mungu [ kuanza na Mungu].

>Maombi ni ishara ya kuhitaji msaada kwa Mungu na imani ni kupokea kwa shukurani uliyoomba mbele za Mungu.

>Ukiisha mwona umpendae huhitaji kuanza kuomba kwa Mungu bali ni kwenda kwa Mchungaji wako ili akupe mwongozo na sura kamili ya mchakato mzima wa kufanikisha safari yako ya ndoa.

ANGALIZO :

Kuna mambo ya kuomba na yapo mambo mengine ya wajibu- yanakutaka kuwajibika; maombi siyo mbadala wa mambo ya wajibu wako. [ Prayer is not a substitute for your Responsibilities].

[iv] Jitoe vema [kikamilifu] kwa ajili ya utumishi.

Neno liko wazi katika Mwanzo 2:15; 29:1-30. Adamu alijitoa vema kuilima na kuitunza bustani ya Edeni ambapo Mungu alimweka na kumpa kazi; hata ikamshawishi Mungu kumtafutia msaidizi wa kufanana naye. Lakini pia tunamwona mtumishi wa Mungu Yakobo anatumika kwa miaka mingine saba zaidi na kuwa miaka kumi na nne ili tu ampate Raheli msichana aliye mpenda, na mjomba wake Labani tunaona anamtoa Raheli na kumpa Yakobo awe mkewe.

-Binti isibweteke tu yaani usikae kwa hasara-mkao wa kuhurumiwa hurumiwa waoaji nao wanaangalia kichwa cha mtu [ufahamu wake na uwajibikaji]; fanya kazi , jishughulishe kwa bidii ili ulete heshima kwenye ndoa yako. Usikalie kupaka rangi kucha na hina na kujipodoa [kujiremba] badala ya kujishughulisha; sio kwamba kujipamba ni vibaya ni jambo zuri sana ila kazi kwanza kisha vipodozi ndio vinafuata.

-Mwanamke anafananishwa na merikebu iliyo jaa shehena-mali; Mithali 31:10-31 na huamka mapema ilikutafuta mali,chakula n.k. kwa ajili ya familia yake.

-Endelea kuwa mwaminifu katika Ibada na huduma [utumishi] na Mungu aonaye sirini na aijuae haja ya moyo wako atakutendea mema.

SURA YA TATU: SABABU ZAINAZOFANYA KIJANA ACHELEW E KUOA AU KUOLEWA.

Zipo sababu nyingi zinazo pelekea kijana wa kike au wa kiume kuchelewa kumpata mwenzi wa maisha yake; zifuatazo ni baadhi tu ya sababu hizo nyingi:-

[ i ] Wengi huwa wamekwisha fanya maamuzi ya nani ataishi naye .
Pamoja na kuwa tayari ana maamuzi yake juu ya mtu wa kuishi naye bado anaenda kumdhihaki Mungu kwa kumwomba ampe mke au mume sahihi wa kuishi naye. Kwa sababu hiyo inakuwa ni vigumu kwao kumpata mtu wa mapenzi ya Mungu na pia inamuwia kazi Mungu kukupa au kukuonyesha mke au mume wa kusudi lake kwani tayari umekwisha kufanya maamuzi ndani ya nafsi yako, hivyo kitu pekee atakacho kifanya Mungu hapo ni kunyamaza tu; utamwomba wala hata jibu utamwita kwa machozi wala hata kusikia. Mithali 16:1-5

[ ii ] Sababu ya kujitamkia maneno ya kinyume [ negative words].

Biblia imeweka wazi kila jambo; nabii bora wa maisha yako ni wewe mwenyewe hivyo uwe makini sana juu ya kile unacho kisema juu yako na wengine kwani maneno yanaumba kwa sababu maneno yote ni roho; Yoh. 6:63. Pia Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazo ya midomo yake.Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. Mithali 18:20-21; Mithali 6:2. Bado Neno linasema wazi kuwa; Maana aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo- Mithali 23:7.Mfano wale wapelelezi 12 waliotumwa na Musa kuipeleleza Kanani 10 wakaja na taarifa mbaya wakisema wao ni wasawa na mapanzi sawasawa na ukiri wao hawakuingia Kanani –Hesabu13:32-33; lakini Yoshua na Kalebu walikataa kuwa mapanzi kwani walimwamini Mungu wao na ndio pekee walioiingia Kanani sawasawa na ukiri wao. Hesabu 14:30.

Eneo hili la kukiri kushindwa limewakwamisha watu wengi bila wao kujua tatizo ni nini; hasa akina dada wengi ndio wahanga wa eneo hili; hii ni kwa sababu mbalimbali kama vile kubakwa, majeraha katika nafsi ya kuachwa au kukataliwa na mchumba au wachumba hata kufikia hatua ya kusema hawataki kuolewa tena au kuoa. Sasa unapita muda wanataka kuolewa au kuoa wanaanza kumuomba Mungu ili awape mume au mke wakati huo wana sahau kwamba kuna kipindi cha nyuma walikwisha kutamka maneno yakujifunga nafsi na shetani kama mwindaji ameyashikilia katika ulimwengu wa roho hivyo ni lazima uende mbele za Mungu kwa toba na rehema ili upate kibali na kisha kuyafuta hayo maneno kwa damu ya Yesu ili kumwondolea shetani uhalali wa kukushikilia kwani bila kufanya hivyo itakuwa ni shughuli pevu kupenya hapo.

[iii] Dhambi.

Neno la Mungu lipo wazi linasema, “ Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atasamehewa na kupata rehema. Mithali 28:13. Kama kuna dhambi kijana amefanya na bado hajaitubia inaweza kuwa ni kikwazo cha kukuchelewesha kwenda kwenye hatima yako njema na kujikuta umri unakwenda, wadogo zako na rafiki zako wanaoa na wengine wanaolewa wewe upo tu.

KUMBUKA:

Kama kuna jambo na silaha pekee anayoitumia shetani kutuzuia kwenda kwenye mema yetu na kumpa adui uhalali wa kutumiliki; ni dhambi isiyo tubiwa. Toba ya kweli hurejesha kibali kilicho potea na ujasiri; kwani dhambi huondoa kibali mbele za Mungu; mtu akitenda dhambi kwenye ulimwengu wa roho anakuwa kama amepakwa mavi, unajuwa wazi hakuna mtu anaye furahia harufu ya mavi kadhalika na Mungu naye haifurahii dhambi. Mfano wapo watu wanao toa mimba au kuwatupa watoto walio wazaa nao kupata mke au mume huwa inakuwa kazi kweli kweli. Hivyo nenda mbele za Mungu ukatengeneze ili upatane kwanza na Mungu. Yakobo 4:7 na Mitali 3:1-4

[iv]. Sababu za kipepo.

Katika kipengele hiki tutaongelea mambo mawili hivi; moja yawezekana wazazi au ndugu wamekwisha mtoa huyo kijana kwa mizimu yao ya ukoo kama dhabihu kwa sababu ya mila zao na jambo la pili yawezekana alipatikana kwa njia za kipepo au za kishirikina [ waganga]. Na hapa nimekutana na kesi hizi mara nyingi kwenye utumishi wangu. Akina dada wengi ambao wazazi wao au wao wenyenye waliwahai kujihusisha na maswala ya mila kama vile kushiriki kwenye sherehe za matambiko na kwenda kwa waganga na hata wengine wakapewa majina maalumu ya kiukoo nakujikuta kwenye wakati mgumu wa kuolewa na mapepo na kuharibiwa hatima zao. Siri moja ni hii yapo mapepo mengine yanapo kuwa yamemwoa binti hayako tayari kukuruhusu kuolewa au kushiriki na mwingine , tendo la ndoa; hivyo lazima yalete upinzani mkali pale utakapo taka kuolewa ili usiolewe au kuoa hasa kama hayo mapepo yamekwisha kufanya tendo la ndoa na wewe ; Lakini habari njema ni kwamba hakuna linalo shindikana kwa Mungu; Kwake yote yana wezekana –Marko 9:23 na kila pando asilo lipanda Baba lazima ling’olewe Math.15:13, Yer.1:9

USHUHUDA:

Nimekutana na mabinti wengi niliyo fanya nao maombi ili kuzizibiti hizo roho za kuingiliwa kimwili na mapepo na Mungu amewafungua wengine tayari wana familia na watoto. Japo awali binti mmoja aliniijia akisema kuwa akisumbuliwa na ndoto mbaya za makaburini analishwa nyama na kubakwa na mapepo usiku; na kila kijana anapokuja kwa lengo la kutaka kumwoa ana mchukia na kumfukuza bila lidhaa yake baada ya kitendo hicho anajutia sana ; kumbe hakujua kuwa yale mapepo ndiyo yaliyokuwa kikwazo cha yeye kuwachukia vijana na kutokuwa tayari kuolewa, lakini baada ya maombi alifunguliwa na sasa yuko huru na ameolewa na ana watoto.

Mwingine huyu yeye alipewa jina la ukoo likiambatana na ibada ya kuchinja mbuzi kama sehemu ya tambiko la kupitisha roho za ukoo ndani yake naye alipata mateso ya kuingiliwa kimwili na mapepo na ndoto za kuongea na wafu na alikimbiwa na wachumba bila kujua sababu za msingi; Binti huyu hakujua kwa nini yanamfika haya mpaka alipotambulishwa kwa Yesu. Mara nyingi mabinti wanaoingiliwa kimwili na mapepo haya huachiwa halufu mbaya inayo waondolea kibali mbele za watu. Ila pamoja na yote hayo yupo Yesu mwenye uwezo wa kurejesha kibali cha ki-Mungu kwako tena. Huyu binti yuko huru sasa kwa jina la Yesu.

[v] Kuwa na vigezo binafsi;

Vijana wengi sana katika swala la kuoa wana vigezo vingi ambavyo wameviweka ni vema kuwa na vigezo lakini uwe tayari kuyaruhusu mapenzi ya Mungu; kwani Mungu ndiye anaye kupa mke au mume. Hivyo wengi hujikuta muda wa Mungu kwa wao kuoa au kuolewa umepita kwani hawakuwa tayari kumsikiliza Mungu bali wao ndio Mungu awasikilize hii ni hatari sana. Tutaangalia jambo hili mbele kidogo.

[vi] Kufanya tendo la ndoa kabla ya wakati.

Mhubiri 3:1- Anasema, “ kila jambo kuna majira yake, na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu.” Swala la kutafuta mke au mume lina majira yake kama wewe ni mwanafunzi nakusihi soma sana tena kwa bidii wakati ukufika wa wewe kuoa au kuolewa itakuwa kama ilivyo pangwa na Mungu ; nimeeleza huko mwanzo kuwa usiyachochee mapenzi wala usi ya amushe mpaka yatakapo ona vema yenyewe . Hivyo usihangaike kutafuta mke au mume utateseka bure endelea na wajibu wako kwa bidii sana kama ni huduma, hudumu sana na kama ni kazi fanya kwa bidii na kama ni kusoma soma sana na Mungu atakutendea mema.

SURA YA NNE: MAMBO YA KUYAELEWA KATIKA MAHUSIANO.
i. Maisha au hali ya mwenzi wako lazima ikuguse ; bila kujali hali,mazingira,mali,elimu,ukoo,kabila n.k

ii. Usimwoe au usiolewe na mtu kwa kumtamani ; kwani ukimtamani binti au kijana lazima utaanguka naye-utazini [utatenda dhambi tu]

iii. Ukimpenda mwenzi wako utamjali, utamuheshimu na kumthamini kwa viwango vya juu; na wala hutasikiliza maneno ya kukuvunja moyo ya watesi –walioshindwa watakayo sema dhidi ya umpendae. Wahenga au wazee wetu walisema, “Akipenda chongo huita kengeza.” Neno nalo linasema, “Upendo hustili wingi wa dhambi.”Maana yake ukimpenda mtu hutayaona madhaifu,makosa na mapungufu yake. Hivyo pendo ni kama kifuniko. Tazama 1Petro 4:8 na 1Kor.13:1-10

iv. Ukiwa mtu wa kuangalia au kuchunguza sana lazima utabagua ; utakuwa mbaguzi [selective];

Kuangalia ni ule uwezo wa kutambua mambo ya ndani [siri] Kama Adamu angeona hali ya ndani ya Eva au Hawa asinge mkubali, maana angeona anguko.[Mambo ya siri ni ya Bwana na yaliyo wazi hayo ni yetu Kumb.29:29]

v. Ukiwa mtu wa kutazama –lazima utapenda na kujali [ kutazama kunashughulika na mambo ya nje ambayo ndio tumejaliwa kuyaona.

vi. Mahusiano yanaanza kwa kutazamana. Rejea Mwanzo 2:18-23.

vii. Hakuna kupenda bila gharama. Kupenda ni kutoa [kupenda kunaambatana na kutoa ] Mfano; Mungu alimtoa Mwanae kuwa sadaka ya ulimwengu kuokolewa; hii inafunua nguvu ya upendo. Tazama Yoh.3:16 nasi tunapaswa kujitoa kwa ajili ya wengine .1Yoh.3:16 na Mwanzo 29:1-30 inaonyesha jinsi Yakobo alivyotumika kwa miaka kumi nne ili kumpata Raheli kama nilivyo eleza hapo mwanzo. Utakuwa tayari wewe kuumia ili umpendae ajisikie vizuri [afurahi]. Kwa mfano utakuwa tayari kutembea kwa miguu au kushinda njaa ili umpendae apande gari au ale chakula. n.k.

viii. Tujenge mahusiano ili tupate akili ya kujuana vizuri. Nilazima umjue vizuri mtu unae fanya nae mahusiano. Kumbuka kipindi cha uchumba ndicho cha kuchimba msingi na kufanya matengenezo ya nguvu sana; ndicho kipindi cha kushughulikia kila aina ya tabia mbovu pengine katika ukoo au mtu binafsi.

ix. Kuna msemo usemao, “Ukimkosa umpendae basi jitahidi kumpenda utakaye mpata.”Maana yake kama wewe unavaa kiatu namba saba ukaenda dukani ukakiona kiatu kingine kizuri ila chenyewe ni namba tatu na ukaamua kujichukulia kwa raha [furaha] zako ukweli kitakubana kisawasawa na kitakutoa sugu na hata kitakufanya kutembea kwako kuwe kwa namna isiyo ya kawaida mpaka utakapo zoea; Hayo ndio baadhi ya maisha ya wanandoa waliopeana wenyewe na sio Bwana, ushauri wangu kwako lidhika na vumilia kwani uliyataka mwenyewe mpaka kifo kitakapo watenga.

x. Weka mipaka [kiasi] katika mahusiano yenu ili msije mkampa ibilisi [shetani] nafasi yakuwatega na kuiharibu misingi kwa kuwa angusha dhambini na kulitukanisha kanisa kwa jamii inayolizunguka; kwa maana sisi ni barua iliyowazi tunasomwa na kila mtu hivyo somekeni vizuri mbele ya mataifa.

xi. Usiwe na mazoea pamoja na mazungumzo [maongezi] yasiyo mpa Mungu utukufu. Biblia inasema, “………Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema; yaani mwenendo wa maisha unakuwa mbovu na mchafu. 1Kor.15:33; Hivyo kijana jiheshimu, jua wewe ni mtumishi wa Mungu na usikae kihasara hasara.

xii. Kijana ukikataliwa na binti au binti ikatokea umektaliwa na kijana basi usimchukie huyo kijana na kumwona mpagani au amepoa kiroho bali wewe mshukuru Mungu kwani amekuponya na tatizo, msiba, janga au mzigo; Zaidi ya yote mpende kama ndugu katika Bwana na kumwombea ili Mungu amkutanishe na jibu lake sahihi, nawe uende ukainue kiwango chako cha Ibada na Utumishi uta mshangaa Mungu atakavyo kutokea na kukujibu kwa moto. Hii ni ajabu utakuta kijana anakuchukua hatua ya kuhama hata kanisa au hata pengine mtaa au mji ati kisa amekataliwa na binti au na mvulana, huo ni utoto ukue sasa upone sasa kwa jina la Yesu.


USHUHUDA:

Ni ushuhuda wa binti mmoja aliye zimia baada ya kuwa kijana amemkataa mbele ya mchungaji wake. Nilimwuliza kulikoni mpaka kupoteza fahamu? Akanijibu akiwa anamshutumu yule kijana akisema, “Yule kijana hajaokoka bali ni mjumbe au wakala [agent] wa shetani anajifanya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu, sikutegemea kuwa angenikataa mbele ya mchungaji wake! Mimi nilimwambia kuwa nimeota ndoto ,nimeona amenishika mkono ananipeleka shimoni [ kuzimu] naona alijisikia vibaya japo mimi sikuwa na maana ya kumwacha bali tuendelee kuikataa hali hiyo; kumbe mwenzangu alichukia na tulipofika kwa mchungaji wake ili kuthibitisha pendo letu kwake; hivyo alipoulizwa kama ananipenda kweli na yupo tayari kunioa, alikataa kabisa kitendo kile kikanisababishia mshituko na kuzimia kwa takribani saa moja hivi.”

>Nami nilimweleza ukweli wote kuwa yule kijana hakua wakala[agent] wa shetani bali yeye –binti ndiye mwenye tatizo kwani hakuwa na ufahamu wakutambua yupi ni chaguo lake sahihi. Hivyo nikamwambia amshukuru Mungu kwani amemponya na matatizo mazito ambayo yangemtesa maisha yake yote ya ndoa. Sasa binti wa watu anasonga mbele kwa amani tele na mipango yake; na huyu kijana naye tayari amekwisha kuoa anaendelea mbele na maisha yake kwa amani nyingi kabisa.

>Hivyo na wewe tulizana usije ukatuletea balaa la kuzimia na pengine usiinuke mwenzako yeye aliinuka na kutupa kazi ya kupepea, tuna mambo mengi ya utumishi na siyo kazi ya kuwapepea watu wasiotaka kujifunza maarifa kama haya.

xiii. Kijana uliyeokoka usijaribu kumtongoza binti na wewe binti usikubali kutongozeka, ukikubali nawe unamatatizo makubwa.

-Kutongoza ni kujaribu kumshawishi binti au kijana akubaliane na jambo asilolitaka na hayuko tayari kulifanya.

*Wewe eleza ukweli wako wote wa maisha usijipachike vyeo , nafasi na majina makubwa [mazito] yanayo kukataa mwisho wake ni aibu na fedheha utakapo umbuliwa kwa ukweli kujulikana.

*Wapagani ndio wanaotongoza [danganya] ili tu wakubaliwe ombi lao.

>Hata leo mabinti nao wana watongoza wavulana [wanawashawishi] kwa namna mbali mbali mfano wanavyoonekana [ mitindo ya uvaaji wa kuacha na kuonyesha sehemu nyeti], mali au fedha n.k; Leo kuna msemo wa vijana usemao, “unanitega” ukimanisha kumshawishi mtu kufanya kitu asichokuwa amekitarajia.


Onyo : Binti wa Yesu vaa vizuri kwa na adabu na heshima zote, jistiri upendeze . Msiwatege vijana kwa mavazi yako ya kikahaba yenyekuonyesha maungo au sehemu nyeti za mwili. Mihtali 7:7-27

Na wewe kijana unayetegwa na ukategeka una matatizo mazito unahitaji msaada wa Mungu wa kufunguliwa ufahamu-akili zako na Bwana na unapaswa kufanya jitihada za makusudi za kuikwepa hiyo mitego kwani ipo wazi.

Rejea kwa rafiki yetu Yusufu ; mtumishi kijana aliye timua mbio mbele ya mke wa bwana wake Potifa

-Mwanzo 39:7-12

xiii. Usioe kwa kumhurumia binti au Usiolewe kwa kumhurumia kijana; tafadhali sana usije ukamkubali mtu kwa kigezo cha kumhurumia; eti kwa madai ya kumpunguzia matatizo au kuondoa kero za kukufuatilia kila mara. Kumbuka hatuoi au kuolewa kwa kigezo cha kuhurumiana bali bali kwa kupendana kidhati na kwa mapenzi ya Mungu.

xiv. Ni vema kuweka vigezo kwa mtu ambaye ungependa awe mwenzi wa maisha yako; mfano ungetaka awe asiye soma,msomi, mrefu, mfupi, mweupe, mweusi, mrefu, mfupi, masikini, tajiri, mwembamba, mnene-bonge, mwenye kitambi n.k. Lakini uwe tayari kuyaruhusu mapenzi makamilifu ya Mungu kuchukua nafasi ya kwanza kwani Mungu kamwe hata kuangusha [hata ku- let down] yeye anamjua vizuri mke au mume atakaye kufaa. Mfano Yesu hakuwa tayari kwenda kufa msalabani lakini katika maombi yake aliyaruhusu mapenzi ya Mungu na mapenzi ya Mungu yakatimizwa yakufa msalabani na kusababisha ukombozi mkuu kwa ulimwengu mzima. Mathayo 26:39-44.

xv. Mke hatuonyeshwi kwenye ndoto bali tunaona waziwazi kabisa kama ilivyokuwa kwa Adamu. Mwanzo 2:19-25; Japo Mungu anaweza kufanya mambo yote , anaweza kukuonyesha kama itabidi au pia akaamua kusema kwa sauti na wewe juu ya huyo umpendae. Ila unapaswa kuwa makini sana kuliko kawaida kwenye eneo la kuonyeshwa na kusema kwa sauti kwani wapo mabinti wengi wameumizwa sana kwa kudanganywa na vijana kuwa ameonyeshwa au Bwana wa majeshi amesema nae juu yake. Zipo sauti nyingi zinazo weza kusema na mtu; mfano sauti ya Mungu, sauti ya Dhamiri na sauti ya Shetani.

USHUHUDA :

Rafiki yangu mmoja aliyedai kuwa Mungu alisema naye kwa sauti zaidi ya mara tatu juu ya binti Fulani nami nikmwambia kwakumtania kuwa hilo ni sembe-yaani shibe tu na tamaa zake, bali aliedelea kusisitiza kuwa Bwana amesema naye kabisa. Chakusikitisha yule binti alimwita kijana huyu ofisini kwake na baada ya kuwa amemnunulia soda huyu kijana asijue anachokiwaza binti huyu; mara binti akafungua kinywa chake na kumwambia kijana akisema, “ Sikupendi na una sura mbaya.”Huyu kijana hakuamini aliyoyasikia. Anasema hakuongea chochote na kama angejua kuwa haya ndio yalikuwa yamejificha kwenye huo wito asinge kwenda ofisini kwake. Kisha yule binti alimpa lift- alimpakia kwenye gari lake mpaka eneo aliloishi kijana huyu. Jakushangaza jamaa huyu aliendelea kudai huyo ndie chaguo lake; mara binti akapata ampendae na sherehe ya kuagwa –send-off ikafika na kufanyika kijana huyu alimwambia Mchungaji wake kuwa huyo binti niwake kabisa na wala ndoa haitafungwa; hayawi hayawi hatimae yakawa siku ya harusi ikafika na yule binti ameolewa na mara ya kufunga ndoa waondoka na mumewe kwenda nchini Marekani lakini pamoja na hayo mtumishi huyu aliendelea kudai kuwa ataachika na atarudi naye atamwoa; chakuchesha baada ya kuona jahazi linazama rafiki yangu huyu akaamua naye kuoa.

Hivyo ana familia yake.

Swali langu napengine na wewe unajiuliza kama mim; Je, huyu aliye sema naye alikuwa ni Mungu kweli? Au ni shetani au dhamiri yake?


SURA YA TANO: UTAJUAJE KUWA HUYU NDIYE CHAGUO LAKO?

Vipimo vipo vingi vyakujua kuwa huyu ndiye aliye umbwa kwa ajili yako; lakini tuangalie kwa kifupi hivi vifuatavyo:-

[i] Amani ya Kristo ndani yako.

-Amani ya Kristo ndani yako ndiyo sauti ya Roho Mtakatifu inayokuthibitishia kuwa upo sehemu sahihi. Filipi 4:7 na Mwanzo 24:56-67-Isaka na Rebeka.

USHUHUDA :

Nikiwa katika moja ya semina ya vijana nikifundisha somo hili katika moja ya Kanisa jijini Dar es salaam; binti mmoja wa Kiganda alinyoosha mkono wakati nafundisha akasema, “Please Pastor let me speak some thing .” [Tafadhali Mchungaji naomba niseme kitu] Nikamruhusu akanza kusema ,”Ni kweli kabisa ulicho kisema Mchungaji, mimi nilimpata mchumba siku tu niliyomkubalia ombi lake kuwa tutaoana nilijikuta na kosa amani moyoni kabisa na nikaanza kumchukia kijana huyu na kila nilipo mwona au kunipigia simu nilijikuta napata uchungu; hivyo nikajua huyu sio chaguo langu ika nilazimu kuanza kufanya maombi ya dharula ya kumtoa moyoni kabisa kwani niliogopa kumwambia sikutani huku tayari nimemkubalia. Nilimwomba sana Mungu anitie nguvu na ujasiri mwingi ili nimwambie aachane na mimi atafute mtu mwingine kwani mimi sina amani moyoni. Tangu siku ile nilipo sitisha mahusiano na mawasiliano ya kiuchumba na kijana huyo nilisikia kuwa na amani tele na furaha kuu moyoni; na kwa sasa sina mchumba lakini moyoni mwangu nina amanitele kwani nimekuwa kama mtu aliyetoka gerezani na bado nina mwamini Mungu kunipa mtu nitakaye mpenda nayeye kunipenda, Amen.-Sambamba na hili kijana mmoja yeye alikuwa amekwisha kulipa mpaka mahari lakini akajikuta anakosa amani na akaamua kusitisha zoezi zima kwani hata ukumbi wa sherehe ya harusi ulikuwa umekwisha kuandaliwa ; pamoja na hayo yote uchumba huo ulikufa na kila mtu akachukua mwelekeo wake yaani kila mtu akachukua njia yake.

- Hivi ndivyo ilivyo usije ukakubali kuolewa au kuoa mtu ambaye huna amani naye moyoni utakiona cha mtemakuni huko ndani ya ndoa; kufa hufi ila cha moto utakipata.KUMBUKA:

Uchumba sio ndoa ; ni bora kuvunjika kwa uchumba kuliko kuvunjika kwa ndoa. Ukikosa amani juu ya jambo Fulani usitafute baraza au kikao au ushauri wa ndugu na marafiki, leo vijana wana msemo wao husema, “Piga chini-yaani achana naye kabisa.”Kuendelea na mahusiano huku ukiwa umekosa amani ni sawa na kujipeleka au kujiingiza mwenyewe jela. Kitendo cha kukosa amani ni sawa na taa nyekundu inayo ashiria hatari, hivyo achana naye mara moja.


[ii] Hata kushinikiza kufanya tendo la ndoa kabla ya kufunga ndoa.

Hatakuwa na haraka wala papara na hofu ya kukukosa [fear of loss].

KUMBUKA: - Tabia ya Mungu ni utulivu-amani.

- Tabia ya shetani ni vurugu-papara au leo vijana wanasema

fasta-fasta - chapuchapu .

Eti utasikia wakisema siwezi kuuziwa mbuzi kwenye gunia, hii ni lugha ya kipepo kabisa achana na mtu kama huyo kwani atakuacha njia panda na kuijeruhi nafsi yako. Mithali 18:14

ANGALIZO:

Binti uliye okoka usije ukakubali kuonjesha au kufungulia chemichem iliyofungwa [kufanya tendo la ndoa] itakuwa ni doa na utapata wakati mgumu wakuifunga tena hiyo chemchemi.

-Usianze mahusiano ya tendo la ndoa [sexal intercourse] kabla ya au nje ya ndoa. Hii ni ishara ya kuwa msingi wa mahusiano yenu sio upendo bali ni tamaa tu.

-Biblia inatoa tahadhali juu ya kuto ya chochea wala kuyaamusha mapenzi hata yatakapo ona vema yenyewe. Wimbo Ulio bora 4:12, 2:7; 3:5.

-Pia mapenzi yanafananishwa na chemichem iliyofungwa, [sealed ] siku itakapofunguliwa itaendelea kutamani kufunguliwa kila siku hivyo yawezekana hata utakapo kuwa ndani ya ndoa utaweza kusubua sana- hutaaminika.

-Ukisha onja au kuonjesha utaendelea kuonjesha na hapo ndipo sasa mwisho wa uthamani na heshima yako- Mpaka umwendee Bwana Yesu kwa toba ya kweli na kwa maombi ya Rehema.

- Tafadhali jitunze, jiheshimu na jithamini ili uimalize safari yako salama na kwa ushindi mkuu.

SURA YA SITA: MAMBO YANAYOVUNJA MAHUSIANO [UCHUMBA].

Yapo mambo mengi sana yanayo vunja mahusiano ya wapendanao au ya wachumba baadhi yake ni:-

[i]. Lugha mbaya [chafu] au Maneno ya hovyo unayo yaongea au kuyasema. Kuna watu hujiropokea na huongea lolote linalokuja. Chunga sana mambo yafuatayo:-

>Maneno unayoyasema au kuyaongea juu ya umpendaye

>Maneno yanayo semwa juu ya umpendaye hata kama watasema maneno ya kumponda-yaani kumsema vibaya kama kweli huyu ni chaguo lako hayo maneno hayata kusumbua hata kidogo ndio kwanza mapenzi yata chanua.

* Kumbuka yawezekana hao wanao mchambua na kumsema vibaya kumbe nao wana mpigia mahesabu au wanataka mkose wote; hivyo uwe macho kabisa.

[ii]. Mwonekano wako/ haiba.

Hapa ni vizuri kijana kuwa msafi [ smart] kiroho na kimwili; usiwe mchafumchafu-hovyohovyo [rough]. Kumbuka usafi ni sifa na tabia ya Mungu [ mbinguni]

-Jifunze kuoga, kufua nguo zako, kupiga mswaki, kunyoa nywele zako sehemu zote zinazotakiwa, kujipaka mafuta na kujipurizia marashi mazuri; sio una mkuta kijana akikupita mbele yako una shika pua kwani anawapa taabu na wakati mgumu kwakuchafua mazingira-yaani hewa [ air pollution]. 1Timo.4:11-12

[iii]. Tabia au Haiba ya asili ya mtu:

Tabia ni somo linalo jitegemea kabisa kwani yapo yale makundi manne ya tabia za watu hivyo ni vema kuijua tabia- yaani mwenendo wa maisha ya huyo umpendaye; watu wengi kwakutokuwa na ufahamu wa tabia za wenzi wao wamejikuta hawamalizi safari zao bali huishia njiani. Mfano wa tabia hizi ni – ukimya, uongeaji, uchangamfu,uongo,ugomvi,wizi. Uzinzi, magonjwa ya kurithi, uchonanishi, utembez i[kiguu na njia], udokozi, n.k.

-Hivyo tabia kama hizi zisipo shughulikiwa mapema kabla ya kuingia nazo ndani ya ndoa itakuwa ni shida tupu kwenye maisha yako ya ndoa. Ni vizuri kila mmoja akawa wazi kwa mwenzake ili kuyaweka mambo vizuri mapema. Mithali 30:11-14.

[iv]. Ahadi za uongo au zisizotekelezeka:

Kuna vijana hutoa ahadi nzito nzito kwa lengo la kukubalika na huyo amtakaye, na atakapo mkubali kwa sababu ya zile ahadi pengine za kumnunulia gari,nyumba , ndege n.k. na inapotokea kuwa ahadi hizo zimeshindwa kutekelezwa husitisha mchakato mzima wa mahusiano. Kumbuka hapo mwanzo niliongea vizuri katika mambo yakuzingatia katika mahusiano kuwa kijana usithubutu kumtongoza binti bali eleza ukweli wako na hitaji lako na usiogope kabisa kukataliwa. 2Yoh1:9-12 na Yoh. 8:43-44, uongo ni tabia kuu ya shetani. Tazama Mathayo 4:1-11 hasa mstari wa 8 unasema, “ Kisha ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia ,Haya yote nitakupa, ukiniangukia kunisujudia.”

[v ]. Sifa au majivuno:

> Tabia ya kujibebesha sifa za uongo ni tabia pacha na ile ya kutoa ahadi za uongo. Leo vijana wana sema, “Kujifanya wa matawi ya juu.” Yaani mtu wa hali ya juu kumbe sio.

> Biblia ina onya juu ya kunia makuu kuliko kawaida. Rumi.12:3. Hebu jitahidi kuwa wewe [ Be your Self]. Utayafurahia maisha kwani hauigizi na utakuishi kwa uhuru zaidi.


[vi]. Mapenzi [kufanya tendo la ndoa] kabla ya ndoa na michezo ya kimapenzi:

Si jambo zuri hata kidogo tena siyo mpango wa Mungu kuanza kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa, Tendo la ndoa limebarikiwa lifanywe na wana ndoa –yaani ndani ya ndoa.

-Pia ni hatari kufanya michezo ya kimapenzi kwani ni sawa na kufanya tendo la ndoa. Mfano kunyonyana ndimi, kutomasana [kushikanashikana sehemu za siri na maeneo yenye kuamusha au kuchochoa hisia za tendo la ndoa], kushika matiti, kiuno n.k. Wimbo ulio bora 2:7 na Isaya 57:4-5. Biblia inasema,” ……msiya chochee mapenzi, wala kuyaamsha , Hata yatakapoona vema yenyewe.”Hapa vijana na mabinti wengi wameumizwa kwa kutishiwa kuwa usipo mpa tendo la ndoa atasitisha mahusiano; nimsema hapo mwanzo mtu kama huyo achana naye ni mharibifu kabisa. Na chakushangaza akifanikiwa kufanya tendo la ndoa nawe wengi wana achwa maana amekipata alicho kuwa anakitafuta. Na mara viongozi watakapo jua kuwa umefanya dhambi ya uzinzi huchukua hatua ya kuku adabisha [ kuku-discipline] na wengi hukimbia makanisa kuepuka aibu na fedheha ; hilo halitakusaidia tulia na kaa chini ili kutengeneza ili uwe na ndoa nzuri.

[vii]. Uchumba wa muda mrefu:

-Si wote waliokaa kwenye chumba za muda mrefu mahusiano yao yalivunjika bali asilimia kubwa ya chumba hizo ziliishia pabaya sana. Nina shuhuda nyingi za kuonyesha kuwa ni hatari sana kuwa na chumba za muda mrefu; kwani mahusiano yao huvunjika vunjika vipande . Mungu hataki upate hasara kwa kukosa maarifa ;Efeso 4:27 anasema,” wala msimpe ibilisi nafasi” hivyo muda mrefu wa mahusiano wengi hujaribiwa na hata wakaona maamuzi waliyo yafanya si sahihi na waka tafuta wenzi wengine. Mfano wengine hukaa miaka 2,3,4.5…na kuendelea pengine kwa sababu ya kimasomo, safari za kikazi n.k.

USHUHUDA:

Ndugu yangu mmoja alikuwa na mchumba wake mara akapata nafasi yakwenda kusoma nje ya nchi huko Uholanzi kwa miaka kama miwili na aliporudi alikuta huku nyuma mwenzake amegeuza mtazamo na kumpata mwanaume mwingine aliye mpenda kuliko. Jambo hili lili muumiza sana ndugu yangualiporudi nchini asijue kinacho endelea; badala ya kutegemea kupokelewa na mpenzi wake kwa furaha lakini kinyume chake akajikuta ana pokelewa na kukataliwa na mtu aliye agana naye kuoana; alikuwa tayari amechukuliwa na mwingine. Kama nilivyo sema mwanzo ukikataliwa mshukuru Mungu kwani amekuponya na tatizo. Sasa ndugu yangu huyu ameoa na ana watoto na wanaishi nje ya nchi kwa sasa; wanafuraha na amani tele.

[viii]. Ukosefu wa mawasiliano:

Mahusiano yoyote hujengwa na kuimarishwa na mawasiliano. Watu husema mawasiliano ni nusu ya kuonana. Kwa hiyo kama kutakuwa na hali ya kupotea na kuvunjika kwa mawasiliano basi kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza mahusiano. Leo wewe ni shahidi tumepotezana na marafiki wengi sana kwa sababu ya kutokuwa na mawasiliano. Hebu rejea kwa rafiki zako wote uliokuwa ukisoma pamoja nao yamkini wengi wao hujui wako wapi na utakuta kuna mipango mliokuwa mkipanga kuifanya wote baada tu ya masomo yenu ; sasa imeyeyuka kwa kukosa mawasiliano.

USHUHUDA :

Kijana mmoja alimpenda binti tuka mwita binti yule tukamketisha chini ili kuisikia kauli yake kama amekubali kuolewa au la; akasema tumpe muda akaombe ili kuthibitisha kama ni Mungu au sio, lakini hakika nilijua hataomba na wala wengi wao wanao sema naenda kuomba huwa; hawa ombi kabisa. Yule kijana akawa anasubiri jibu bila matumaini hasa pale namba ya simu ya binti huyo ilipo acha kupatikana kila alipopigiwa hii ilimfanya kijana kusalimu amri nakuanza mchakato mpya na sasa amempata ampendaye na mwasilianao yanaendelea na maendeleo ni mazuri sana. Hivyo utakubaliana na mimi kuwa mahusianao ni mawasiliano. Amos 3:3 na Mwanzo 11:1-9. Silaha pekee aitumiayo adui ni kukata mawasiliano ili msiwaliane na kujenga nguvu ya pamoja.

[ix]. Usaliti [ betrayal]:

Hiki ni kitendo cha kuvujisha siri au kuwa kinyume na makubaliano-[ ni kuwa adui].

Mara nyingi usalti hutokea au husababishwa na tama ya mali na hofu ya maisha hasa pale wapenzi hawa wanapokuwa mbalimbali na kukosa mawasiliano, hivyo adui huingilia kati na kuwagawa hawa wachumba na kuwasambalatisha kabisa. Yoh.6:70.

[x]. Utofauti wa Imani :

- Vijana wengi walioko nje –duniani hutamani sana mabinti walioko ndani- waliookoka; hivyo baadhi ya vijana hukubali kuokoka kwa lengo la kumpata binti na akisha mpata ndio mwisho wa mchezo binti anakuwa ameumizwa na hapo mahusiano yao huingia matatani na hata kuvunjika kabisa; Hii ni kwa sababu kijana au binti alikuwa mpagani wakawaida tu. 2Kor.6:14-18- Msifungiwe nira pamoja na wasio amini, kwa jinsi isivyo sawasawa…….hakuna ushirika kati ya giza na nuru.

SURA YA SABA: MAMBO YANAYO JENGA UHUSIANO.

-Tumeona mambo kumi ya yanayopelekea kuvunjika kwa mahusiano na kinyume mambo hayo yana jenga mahusiano; pamoja na haya machache yafuatayo:-

[i] Ukweli uadilifu na uaminifu: Yoh.8:31-33 , 1Sam.16:7 na Math.5:37

Biblia insema kweli yenu iwe kweli na siyo yenu iwe siyo; maana yake; ni kusimamia unacho kisema [walking your talk] yaani kumanisha unachosema na kusema unacho maanisha.

Kumbuka uadilifu unahusika na tabia [moyo] wa mtu; uadilifu unajengwa na kutenda,kutekeleza ahadi na kujitoa kikamilifu.

KUMBUKA: Unapo poteza uadilifu unapoteza uthamani na ubora wa ujana wako.

[ii]. Mawasiliano: Amos 3:3

Wazee walisema mawasiliano ni nusu ya kukonana, kwa hiyo mahusiano yana jengwa kwa mawasiliano na kama hakuna mawasiliano hakuna mahusiano, maana hamtaweza kutembea njia moja mpaka muwe mmepatana kwanza.

[iii]. Lugha au Maneno mazuri:

-Chunga sana unacho kisema mbele ya mwenzi wako mtarajiwa kwani ukiongea unampa nafasi ya kukuthaminisha na kukupima uwezo wako wa ufahamu. Kuna vijana wanajua kuongea vizuri na wengine walopokaji tu ; hivyo kijana fikiri kabla ya kuongea uwapo mbele ya huyo umpendaye.

USHUHUDA:

Kijana mmoja alimchumbia binti na kabla binti hajatoa jibu la ndio au hapana , kijana akawa ana mshinikiza kutoa jibu huku akiropoka nami nikisika kuwa ,”Tazama naendelea kukonda tu , wala hunijali mtu unapendwa lakini haupendeki; kama hunipendi na hunitaki niambie mapema kwani mabinti ni wengi sana usinisumbue kwa kukubembeleza bwana.”Huo ni utoto ni kukosa misingi ya mahusiano kama hii. Ukweli binti alimkataa baadae kwani kijana alikuwa akiongea kama kameza kanda [anaongea sana] na binti yeye alikuwa mkimia tu akaamua kukataa kwani aliyaona matokeo ya ndoa yake mapema kabla ya ndoa yenyewe.

USHUHUDA WANGU BINAFSI:

Wakati na majira yalipowadia Mungu kunipa mke wangu kipenzi na chaguo la Mungu kwa ajili ya moyo wangu; nilipomwendea sikuwa na maneno yenye mbwembwe na madowido nilinyoosha maneno wala sikutafuna wala kumumunya maneno.Nilimwambia wewe ndiwe utakaye kuwa mke wangu na mzazi mwenzangu wa maisha tuzae watoto na kumtumikia Bwana Yesu na hivyo ndivyo ilivyokuwa hata sasa.

[iv]. Uaminifu: 1Kor.4:1-2,Zab.51:6 ,Luka 12:42-48

Mungu ana pendezwa na kweli iliyo moyoni; hivyo hata huyo umpendaye atakapo uona uaminifu wako kwake pendo litakuwa kuu sana. Kuna wanandoa wanaishi maisha ya kuchungana kama kuku mgeni; yaani hawa aminiani hata kidogo. Njia pekee yakumjua kuwa mtu huyu ni mwaninifu ni kumwamini.

KUMBUKA:

Hutaweza kumchunga binadamu kiumbe chenye akilli bali ni Mungu pekee ndiye awezae kumlinda na kumchunga.

[v]Mwonekano mzuri au usafi [smartness]:

Kama nilivyo eleza hapo mwanzo kuwa binti au kijana usijitelekeze mpaka ukawa kero kwa uchafu wa kiroho na kimwili. Jitunze vizuri,vaa vizuri na upendeze vizuri.

- Hakuna mtu anayependa kukaa na mtu mchafu.

KUMBUKA :

Hata mtu mchafu na na yeye hampendi mtu mchafu. Hii ni ajabu na inafurahisha kweli.

[vi]. Imani moja: Amos 3:3

Mkiwa na imani moja wote, Mungu mmoja,ubatizo mmoja, mbingu mmoja zoezi huwa rahisi pengine tu asiwe chaguo lako- siyo ubavu wako.

[viii].Uwezo wa kujitawala au kiasi: Galatia 5:22

Ni jambo la muhimu sana kwa kijana au binti kuweka mipaka katika mahusiano. Ni vema kujua kuweka mipaka; wapi uongee na wapi usiongee. Lakini utakuta vijana hawana breki- mipaka, wanajiachia tu; hebu jaribu kujitawala kwani mwenzako ana kusoma hatua kwa hatua.

SURA YA NANE: MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUIMALIZA SAFARI YA MAHUSIANO SALAMA NA KWA USHINDI MKUU:

Yafuatayo yatakuwa ya msaada kama tu yatazingatiwa:-

[i]. Uwe na kiasi [self control]- Gal.5:22

-Kijana ukiwa na uwezo wa kujtawala basi utapenya katika safari au mwendo salama.

Weka mipaka katika maeneo yafuatayo:-

*Achana na Mazungumzo mabaya; Mazungumzo yasiyo na maana yatakayo kupelekea kumkosea Mungu. 1Kor.15:33.

* Kutokuwa na mazoea yakupitiliza kati ya kijana na binti; Si jambo la busara kwa kijana na binti kufanyia maongezi mafichoni [ gizani ] kama vile mna ibana. Hii inaweza kupelekea ajali ya kuanguka dhambini; kwa kufanya ngono au tendo la ndoa nje ya ndoa.

* Usijirahisi eti kuonyesha unampenda mwezi wako mtarajiwa.

“Uwe rahisi kuingilika lakini siyo kujirasi” [ Be simple but not Cheap]

[ii].Uwe na maono au ndoto: Mithali29:18

-Mtu mwenye maono ana mipango, malengo na mikakati katika mambo yake; hajiendei endei hovyo hovyo.

* Panga unataka kuishi maisha ya namna gani? Wapi? n.k

KUMBUKA:

Vijana wengi wanao anguka yaani kufanya dhambi ni kwa sababu wapowapo tu hawana maono,hawana mipango wala mikakati wamebweteka tu [ idol]. Hivyo kwa kuwa hawana mipango shetani huwapatia cha kufanya ; mfano kazi ya uzinzi –Mith.6:32. Watu husema akili isiyojishughulisha ni kalakana ya shetani [ idol mind is the work shop of the devil].

[iii]. Jaa Neno na Roho Mtakatifu: Luka4:1-15; Kol.3:16.

Neno la Mungu ni silaha tosha katika kuzipinga hila za shetani ; maana Neno ni upanga mkali ukatao kuwili…..na Roho Mtakatifu atakufundisha na kukuongoza ili usifanye makosa.

[iv]. Kimbia au ondoka maovuni: Mwanzo29:5-23

-Mtumishi wa Mungu Yusufu, alichukua hatua ya kukumbia pale alipotakwa kwa nguvu kimapenzi; akakataa na akaamua kukimbia baada ya kukoswa koswa kubakwa na mke wa bwana wake Potifa mke wa Farao.

KUMBUKA:

Usijifanye kuwa wa kiroho kuliko au kupita Neno la Mungu-biblia utaumia. Kulifanya jambo lisilo la kiroho kuwa la kiroho ni kuuficha ukweli uliokusudiwa kujulikana.

-Utashangaa kuona kijana na binti si wana ndoa ni wachumba tu anashinda chumani mwa kijana tena anakaa kitandani na ikibidi kujipumzisha kabisa pamoja na kumpikia chakula; kupika si dhambi ila sio wakati wake subiri ufunge ndoa . Kumbuka upo mwilini na kijana na binti ni sawa na hasi na chanya kwa kukosa nidhamu ya kuweka mipaka lazima kutatokea kishindo cha mlipuko wa hatari. Hapa hukatazwi kuongea na mwenzako ila unafanyia wapi hayo maongezi. Nini usalama wa mazingira hayo? Jitahidi kufanyia maongezi yenu katika maeneo yalio wazi ili adui asije akapata nafasi ya kuwa maliza. Pia mtakuwa salama dhidi ya wachafuzi na wachongezi.

[v]. Fanya maombi : Luka 18:1-8

Kumbuka uchumba sio ndoa bali ni safari kuelekea kwenye ndoa hivyo unatakiwa kufanya maombi ya ulinzi wa mahusiano yenu kwani adui hata waacha hata kidogo atahakiksha anafanya awezalo ili kuwakwamisha ; lakini kama mtadumu katika kumatafuta Mungu na nguvu zake lazima mtafanikiwa tu. Ni sawa na mama aliye mja mzito, asipokuwa macho uja uzito utaharibika na kama akijifungua vizuri haitoshi lazima amuhudumie mtoto mpaka aweze kujitegemea mwenyewe.

KUMBUKA: 

Kupokea muujiza ni kitu kingine na kuutunza muujiza huo ni jambo jingine kabisa; tuna pokea vitu vingi lakini havipo leo kwa sababu hatuna ufahamu wa kuvilinda ili vidumu.
Kuwa na kitu haimaanishi unakimiliki; unaweza kuwa na mchumba na mtu mwingine akaja aka mmiliki [kumwoa]- [ To own does not mean to possess.] Rejea kwa Adamu hakusimama kwenye nafasi/zamu yake ili kuilima bustani na kuitunza maana yake ni kuilinda; shetani hakumchelesha alimoa bustanini kwa kumkosanisha na Mungu kwa kuto kutii maagizo ya Mungu. Tazama Mwanzo 2:15-17 na Mwanzo 3:1-24 hasa mst 23.

USHAURI:

Ipo siku utashangaa huyo huyo mpenzi wako umpendaye atakuumiza na hata kusababisha mtikisiko mkubwa kwenye moyo wako na hata kukufanya ulie kama mtoto; isikusumbue hata kidogo kama ni chaguo lako toka kwa Mungu lazima vita iwe kali sana kuhakikisha shetani ana pingana na kusudi la Mungu kutimia kwako. Usikate tama songa mbele kwa imani huku ukimwomba Mungu siku zote ili kuimaliza safari yenu salama na kwa ushindi mkuu. Ukweli ukiwa vizuri na Mungu shetani hataweza kuwatikisa wala kuwashinda kwani tumehakikishiwa ushindi na Bwana Yesu katika Mathayo 16:18-19 na Warumi 8:31-33.

SURA YA TISA: MAOMBI:

*BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO NINAKUSHUKURU KIPEKEE SANA KWA KUNIPA UFAHAMU NA MAARIFA KWANI NDIWE UNIFUNDISHAE ILI NIPATE FAIDA NAKUSHURU KWA AJILI YA MTUMISHI WAKO ULIYE MTUMIA ILI KUNIPA MAARIFA HAYA MAANA HUTAKI NIANGAMIE KWAKUKOSA MAARIFA KAMA USEMAVYO KATIKA HOSEA 4:6 NAMI NITAWASAIDIA WENZANGU ILI WASIJE KUANGAMIZWA NA ADUI;MUNGU NISAIDIE NA KUNITIA NGUVU NA KUNIWEZESHA KUYAFAHAMU HAYA NA KUYATII ILI MWISHO WANGU UWE MZURI KATIKA JINA LA YESU, AMEN.

MWISHO:
Nina imani kuwa somo hili limekuongezea ujuzi,maarifa na ufahamu wa kutosha kukusaidia katika kuenenda katika mapenzi ya Mungu kwa kipindi chote cha mahusiano au uchumba wenu. Nawatakia baraka za BWANA na USHINDI MKUU katika kipindi chenu cha uchumba na hatimaye mkawe na NDOA YENYE UTUKUFU WA MUNGU, AMEN.

UISHI MILELE- 2KOR. 13:14

MAWASILIANO:

ANUANI YA MWANDISHI:-

Pastor. Songwa .MM. Kazi

Tanzania Assemblies of God

TAG KONGOWE FOREST

S.L.P 70983, DSM

Simu: 0757-567 899, 0789-567 899,

0774-567 899 na 0719-968 160.

Email: ptrsongwak@gmail.com

songwak@yahoo.com

pkazi@mail.com

Blog: lcm2014.blogspot.com

1 comment:

karibu kutoa maoni | your comments are welcomed